Staa wa nyimbo za aina ya Ohangla Lady Maureen Achieng' aliruhusiwa kuondoka hospitalini Februari 20 baada ya kupata nafuu.
Habari Nyingine: Mshukiwa wa utapeli afumaniwa JKIA akihepa nchini

Lady Maureen amekuwa akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga kwa muda wa mwezi mmoja.
Hata hivyo, msanii huyo alikuwa hana makazi kwani familia yake akiwemo mama mzazi ilimkana ila kwa sasa amepata msamaria mwema.
Kulingana na ripoti ni kuwa, Maureen amechukuliwa na mpwa wake ambaye amejitokeza ili kumsaidia apate angalau mahali kulala akiendelea kupata nafuu.
Habari Nyingine: Makachero wamkamata jambazi sugu anayewahangaisha wakazi wa Nairobi

“Nimechoshwa na kukaa maeneo haya. Naomba msamaria mwema yeyote anitoe hapa. Bado nawapenda wote,” Maureen alisema.
Kulingana na taarifa ambazo TUKO.co.ke imezipata, familia ilimkana msanii huyo baada ya mzozo wa nyumbani kuzuka miaka kadhaa iliyopita.
Habari Nyingine: Uporaji uliofanyiwa Wakenya wakati wa kukubali mradi wa SGR

Awali, mwanamuziki Esther Akoth almaarufu Akothee alimlipia bili ya hospitalini baada ya habari kuhusu hali yake mbaya kiafya kuenezwa mitandaoni.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaX94hZhmmaKml6yubsPAZqahmZ6cuaJ5y5qbsmWdlsKzscSnZJqkma6yrK3TmqOir5Fiu6J5zJqkmmWdr667tYyap5qskWK6orfAqGWhrJ2h