DCJ Philomena Mwilu, DP Ruto na Seneta Linturi wakamilisha masomo UON

- Naibu Jaji Mkuu atahitimu kwa kupewa cheti cha uzamili Chuo Kikuu cha Nairobi, pia Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa atapewa cheti cha uzamili katika Sheria - Seneta wa Meru anayekabiliwa na utata Linturi hatimaye atapewa shahada ya Sheria baada ya taasisi hiyo kumwondoa katika sajili yake 2017

- Naibu Jaji Mkuu atahitimu kwa kupewa cheti cha uzamili Chuo Kikuu cha Nairobi, pia Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa atapewa cheti cha uzamili katika Sheria

- Seneta wa Meru anayekabiliwa na utata Linturi hatimaye atapewa shahada ya Sheria baada ya taasisi hiyo kumwondoa katika sajili yake 2017

- Naibu Rais William Ruto naye atapata cheti cha Uzamifu (Ph.D) kuhusu Mimea Mazingira

Naibu Jaji Mkuu (DCJ) Philomena Mwilu ataungana na Naibu Rais William Ruto na viongozi wengine wawili katika sherehe za kufuzu Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN).

Habari Nyingine : Video: Wakenya wampigia saluti binti Mkorino aliyesakata densi katika harusi yake

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Seneta wa Meru anayekabiliwa na utata Mithika Linturi, pia atakuwa miongoni mwa maelfu watakaohitimu na atapewa shahada ya Sheria baada ya taasisi hiyo kumwondoa katika sajili yake 2017.

Ripoti ya Daily Nation ya Alhamisi, Disemba 20 ilisema kuwa, Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa naye atapewa cheti cha uzamili katika Sheria kwenye sherehe hizo.

Habari Nyingine : Raila Junior amshambulia DP Ruto kuhusiana na katiba ya sasa

Wakati Naibu Rais William Ruto atakapokuwa akipewa cheti cha Uzamifu (Ph.D) kuhusu Mimea Mazingira, DCJ atakuwa akipewa cheti cha uzamili katika Sheria.

Ruto alifanikiwa kutetea mchanganuo wake Oktoba 24 na 25, 2018, na hatimaye kuwekwa katika orodha ya mahafala baada yamuda mrefu akikosa kuhitimu.

Habari Nyingine : Jamaa amfurusha mkewe siku 2 baada ya harusi, adai mtu aliifungua 'sava'

Kuhitimu kwa Linturi ni habari njema hasa baada ya yeye na chuo hicho kuhusika katika kesi kortini kufuatia chuo hicho kumwondoa katika sajili yake kwa kudai aliwasilisha stakabadhi feki wakati wa kusajiliwa katikataasisi hiyo.

Linturi alkishtaki chuo hicho na kusema kilikuwa kikihusika katika kumwangusha kisiasa kwa ushirikiano na wapinzani wake ambao aliwataja kuwa aliyekuwa Gavana wa Meru, Peter Munya na Milton Mugambi Imanyara.

Habari Nyingine : Serikali ya Migori yapuzilia uwepo wa ugonjwa mpya hatari wa zinaa ‘Jakadala’

Wanne hao watakuwa miongoni mwa maelfu ya wanafunzi watakaokuwa wakihitimu katika sherehe za 60, Ijumaa, Disemba 21.

Ruto pia atakuwa akiadhimisha kuzaliwa kwake vilevile harusi yake ambayo ilifanyika tarehe hiyo.

Read: ENGLISH VERSION

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke ,kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiboF1fpNmm5yiXaW1qrjOppynmV2ixKq41GabqWWiqsGwec2aZKydnprBonnLoqWtraKeeritypqkoqSZqLWiecyaqqiln2LCsLqNoaumpA%3D%3D

 Share!