Donald Trump na Kim Jong Un wakutana ana kwa ana Singapore

Mkutano wa kihistoria uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore. Kwa mujibu wa ikulu ya White House, Jumanne, Juni 12, wawili hao walikutana pekee yao kwanza kwa dakika 38 na kwenye mkutano wao, hapakuwapo na watu wengine ila wakalimani

Mkutano wa kihistoria uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.

Kwa mujibu wa ikulu ya White House, Jumanne, Juni 12, wawili hao walikutana pekee yao kwanza kwa dakika 38 na kwenye mkutano wao, hapakuwapo na watu wengine ila wakalimani wao.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Orodha ya makanisa 5 tajiri zaidi nchini Kenya

Kulingana na BBC, Bw Trump alisema walipiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka ya makubaliano.

Pia alisema Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama kasi ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia, na baadaye walitia saini waraka wa makubaliano.

Habari Nyingine: Mkenya adanganya Wazungu ‘lamba lolo’ ni salamu, waanza kuimba (video)

Mkutano huu ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel ya kisiwa cha utalii cha Sentosa, kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.

Singapore ni nchi ya tatu ambayo Kim Jong-un ameitembelea tangu kuanza hatamu yake mwaka wa 2011.

Habari Nyingine: Mwanamume afumaniwa akijifanya mwanamke kuwanyemelea wanaume wenzake (picha)

Kwanza Kim ilizuru China mwezi Machi na mwezi Aprili akawa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kutembelea Korea Kusini na kufanya mashauriano na Moon Jae-in.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIN2gZFmm6imkaGxbsDRrqSpZZ6Weqy1zGahqKaXYsKvedaaoq6skaOubq3NmmSkr5Firq%2BtjKygp5%2BRpbyzsY2hq6ak

 Share!