Nimekomaa na kuwa mtu mzima, wapiga kura wa Nairobi wanafaa kuniamini- Mike Sonko

-Mgombea wa kiti cha ugavana wa Nairobi Mike Sonko alisimulia jinsi mienendo yake imebadilika tangu alipopata shahada -Sonko alisema jinsi alivyopenda vurugu na sasa amekomaa kiakili na kimaadili Seneta wa Nairobi, na mgombea wa kiti cha ugavana wa Nairobi,Mike Sonko ameelezea jinsi alivyobadilika baada ya kupata shahada ya chuo kikuu.

-Mgombea wa kiti cha ugavana wa Nairobi Mike Sonko alisimulia jinsi mienendo yake imebadilika tangu alipopata shahada

-Sonko alisema jinsi alivyopenda vurugu na sasa amekomaa kiakili na kimaadili

Seneta wa Nairobi, na mgombea wa kiti cha ugavana wa Nairobi,Mike Sonko ameelezea jinsi alivyobadilika baada ya kupata shahada ya chuo kikuu.

Habari Nyingine: Zari afichua KILICHOMUUA mume wake wa zamani, sio sumu

Akiwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio pamoja na mpinzani wake kwa ugavana wa Nairobi Evans Kidero, Sonko alisema kuwa kurudi kwake shuleni kulimlazimu kubadili tabia na mienendo yake.

“Nilikuwa najulikana kwa kupiga ukuta makonde lakini sasa nimebadilika na ninatosha kuwa gavana wa Nairobi. Nilisoma mambo mengi shuleni ambayo yalinifunza kudhibiti hasira yangu,”Sonko alisema.

Habari Nyingine: Mumewe Size 8 - DJ MO - ana watoto wengine nje ya ndoa? Pata uhondo (picha)

Seneta huyo wa Nairobi bila shaka anajulikana kwa hasira yake ya haraka hasa anapopambana na masuala yanayowakumba wenyeji wa Nairobi.

“Kwa sasa nimekuwa mtu mzima baada ya kuenda shule na baadhi ya masuala niliyosomea ni maadili na uongozi mwema,” Sonko alisema.

Habari Nyingine: Wafuasi wa Joho wamgeukia na KUMSUTA kwa njia ambayo itamchukua muda kusahau

Kulingana na mwanasiasa huyu tajira na mweye ukarimu wa hali ya juu, shahada aliyopata bila shaka inamfanya kuwa mwanasiasa tofauti na wapiga kura wa Nairobi wanafaa kumuamini.

Tazama video ifuatayo kwa habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaYB1hJFmpaKllaC8rq3AZqWaZZuqxKJ5zK2sZqWqnrqiedaap6KfkWK4tr7AZq6aZZ6WtrO7waJksJmelrOirYykrKehkaK2r7WMpqCknV2ovG%2B006aj

 Share!